Stori: Erick Evarist, Risasi Jumamosi
DAR
ES SALAAM: Uchumba wa staa wa wimbo wa Chura, Snura Mushi na mwanaume
aliyetajwa kwa jina la Ally umevunjika kabla hata wazazi wa msanii huyo
hawajatoa majibu ya barua ya posa.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, kuvunjika huko kunatokana na muoaji huyo
kumweleza wazi Snura kuwa, katika maisha yao ya ndoa, yeye hatahusika na
matunzo ya watoto wawili ambao staa huyo wa muziki amezaa na wanaume
wengine.
“Ndiyo
kwanza huyo Ally alikuwa amepeleka posa nyumbani kwa wazazi wake Snura,
Mwananyamala (Dar) na ilishapokelewa, alikuwa akisubiri jibu ili kama
wakikubali aoe, lakini kwenye uchumba wao ndiyo akamwambia mwenzake
hivyo, naye akaona hawezi kukaa na mwanaume ambaye hawataki watoto
wake,” kilidai chanzo hicho.
“Kumbe
hamjainyaka hii habari? Iko hivi kuna jamaa anaitwa Ally ndiye
alimchumbia Snura. Alimtuma mshenga wake anaitwa HK (meneja wa Snura)
kwenda kumuwakilisha katika suala zima la kutoa posa,” kilidai chanzo
hicho huku kikiomba hifadhi ya jina.
Chanzo
hicho kikasema: “Lakini sasa uchumba umevunjika na hakuna ishu tena.
Hii ni kama mkosi kwa Snura japokuwa hata mwenyewe Snura alikuwa radhi
kwa sababu alizosema jamaa.”
Baada
ya kunasa ubuyu huo, Risasi Jumamosi lilimvutia waya HK ambapo
alipopatikana alikiri kwenda kutoa posa na kuongeza kwamba, uchumba huo
ulivunjika muda mfupi baada ya jamaa kuweka wazi kwamba, anamtaka Snura
tu na si watoto wake.
Mama Snura
“Si
unajua misimamo, jamaa alitaka kuwa na Snura na si watoto, Snura akaona
hawezi kuwatupa watoto wake, anataka kuwalea mwenyewe, na yeye akasema
uchumba ufe tu,” alisema HK.
Alipoulizwa
Snura kuhusu tukio hilo, alisema alipokea kwa mikono miwili uchumba huo
lakini alishangaa msimamo wa mtarajiwa wake huyo wa kutotaka watoto.
“Kuolewa
ni jambo la kheri lakini watoto pia ni baraka. Sasa kama mwenzako
hataki watoto wako nini kitaendelea? Hata mimi sikuwa radhi, uchumba
ukafa,” alisema Snura.
Kabla
ya kuchumbiwa na Ally, Snura alishazaa na wanaume wawili tofauti ambao
wote safari yao iliishia njiani baada ya kumwagana kwa kushindwana
tabia.
0 comments:
Post a Comment