Matukio ya Dodoma
Samson
Joramu(44), mkazi wa Chololo, Kata ya Kikombo, alimchinja mke wake,
Rehema Joram (43) kabla ya kujiua kwa kunyonga katika shamba lake.
Watu
walioshuhudia walisema, Joramu baada ya kumuua mkewe alijinyonga na
aliandika ujumbe uliokutwa mfukoni kwake, ukisomeka: “Mama tunza
wanangu, mimi nimekufa.” Kadhalika aliandika orodha ya watu anaowadai.
Katika
tukio jingine, Amos Kalenda, mkazi wa Kikombo, Dodoma anadaiwa kumuua
mama yake mzazi, Joyce Kalenda kwa kumchinja. Chanzo cha mauaji hayo
kinadaiwa ni mama huyo kumnyima chakula.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa akizungumzia tukio hilo
alisema kuwa: “Ni kweli taarifa za vifo kutoka Kikombo ninazo, yule
mmoja alimuua mama yake kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili jana
(juzi), na huyu mwingine alimuua mke wake asubuhi ya leo (jana) kisha
naye akajinyonga,” alisema.
Tukio la Tarime
Mkoani
Mara katika Wilaya ya Tarime, Wambura Mariba (50) mkazi wa Matongo,
Nyamongo, Tarime, anadaiwa kumuua kwa kumchinja mkewe, Maria Wambura(40)
kwa madai anamroga.
Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Andrew Satta alisema tukio hilo lilitokea Juni 8 saa tisa alasiri.
Satta alisema baada ya mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, alichoma moto nyumba zao mbili, zilizokuwa zimeezekwa kwa nyasi.
“Baada
ya tukio hilo kutokea, wananchi walijichukulia sheria mkononi na
kumjeruhi mtuhumiwa kichwani na kitu chenye ncha kali,”alisema Satta.
Wakizungumzia
tukio hilo ndugu wa marehemu, Samwel Wambura alisema tukio la mwanamke
huyo kuuawa, lilitekelezwa mbele ya watoto wake wakati akiwaandalia
chakula.
“Alipomaliza
kumuua, alianza kuandaa moto achome nyumba ili mwili wa mkewe uungulie
ndani, majirani waliwahi kuuchukua mwili, lakini alianza kuwafukuza huku
akiwa ameshika panga,” alisema na kuongeza: “Wananchi baada ya kuona
tukio hilo walipiga simu kituo cha polisi ambao walifika na kumkamata
mtuhumiwa.”
Mganga
Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto, Kagumiwa Kaijage alisema, alipokea
mwili wa marehemu ukiwa umekatwa shingoni na mtuhumiwa amelazwa
hospitali hapo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali mwilini.
0 comments:
Post a Comment