Dodoma:
Watanzania 408 wanatumikia vifungo nje ya nchi na wengine kukabiliwa na adhabu ya kifo baada ya kusafirisha dawa za kulevya.
Taarifa
hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga alipokuwa
akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha
2016/17.
Akizungumzia
Watanzania waliokamatwa kwa dawa hizo Mahiga amesema wanakabiliwa na
adhabu hizo katika magereza mbalimbali duniani baada ya kukutwa na hatia
ya makosa ya kujihusisha na biashara haramu.
Mahinga
alitaja idadi yao na nchi ambazo wanashikiliwa kuwa ni Brazil (41),
China (266), Iran (68), India (9), Nepal (4), Oman(3), Thailand (14) na
Umoja wa Falme za Kiarabu (3).
0 comments:
Post a Comment