Rais Magufuli tunakuunga mkono kwa dhati kupambana dhidi ya ufisadi. Tunakupinga kwa nguvu zote kupambana dhidi ya demokrasia.
Kuanzia
mwanzo tumekuunga mkono dhidi ya ukwepaji kodi, ubadhirifu, uvivu na
uzembe. Tangia mwanzo tulionya kuwa ni lazima udhibitiwe na Bunge ili
ufanye kazi kwa mujibu wa Katiba. Hivi sasa wewe Rais ndio unaendesha
Bunge kwa remote control.
Tutakupinga kuturudisha nyuma. Hutafanikiwa
kamwe kubomoa misingi ya taasisi za uwajibikaji tulizoanza kuzijenga.
Narudia
nukuu muhimu sana " ukitaka kutawala tawala peke yako. Ukitaka kuongoza
ongoza na wenzako". Rais Magufuli Tanzania inataka uongozi madhubuti na
sio itawapendeza wa imla. Huko tumeshatoka na Watanzania hawatakubali
kurudi huko.
Haya kayaandika kwenye ukurasa wake wa Facebook

0 comments:
Post a Comment