Mtu
mmoja amefariki dunia na mwingine amejeruhiwa vibaya katika ajali ya
gari iliyotokea wilayani Kilwa mkoani Lindi baada ya magari mawili
kugongana uso kwa uso.Taarifa ya jeshi la polisi mkoani Lindi
imeeleza kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kisangi katika kijiji
cha Mkwanyule kwenye barabara ya Kilwa Lindi ambapo gari yenye nambari
za usajili T 556 Suzuki Carry iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Hijra Said
Abdurahman ambae alifariki hapohapo baada ya gari yake kugongana uso
kwa uso na gari nyingine Toyota Corolla yenye nambari za usajili T 840
Bug iliyokuwa inaendeshwa na Ahmad Mohamed Mfaume ambae amejeruhiwa
katika paji lake la uso.Mkuu wa wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai amezungumzia kuhusu ajali hiyo na akatoa wito kwa madreva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kukomesha matukio ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara na kusababisha vifo vya raia na uptevu wa mali.
0 comments:
Post a Comment