Mpiga picha wa Gazeti la Tanzania Daima, aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Mwangosi Joseph Senga enzi za uhai wake.
Na Dotto Bulendu
NI
simanzi na majonzi, siku moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Iringa
kumhukumu kifungo cha miaka 15 askari aliyemuua mwandishi Daudi
Mwangosi, tasnia ya habari imepata pigo kwa kuondokewa na mpiga picha wa
Gazeti la Tanzania Daima, aliyepiga picha za tukio la mauaji ya
Mwangosi, SHUJAA JOSEPH SENGA, aliyefariki dunia jana usiku.
Senga amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Mojawapo ya picha za tukio la mauaji ya Mwangosi alizopiga Joseph Senga.
Bila
Joseph Senga, shujaa aliyehatarisha maisha yake, akasimama bila woga,
akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi wenye silaha,
huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi, milio ya
risasi ikisikika na kuzitunza, zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi,
leo hii asingekuwa Senga, nadhani kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu
dhidi ya aliyemuua Mwangosi. Nakulilia Senga.
Daudi Mwangosi enzi za uhai wake.
Senga,
Senga, Senga, Senga, umekwenda, Mungu aliamua akuweke hai mpaka hukumu
itoke na mwisho amekuchukua, Senga umekwenda wadogo zako katika tasnia
tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.
Senga,
Senga, kamsalimie Daudi Mwangosi, mwabie aliyemuua naye kahukumiwa jela
miaka 15, kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu.
Nenda Senga, picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.
0 comments:
Post a Comment