Baba Yoyoo akimgombeza mwenzake baada ya kuchafua mazingira.
KELVIN SHAYO NA HILARY DAUDI, RISASI mchanganyiko
DAR
ES SALAAM: Mmasai mmoja mwanaume, ambaye sehemu za mijini wanafahamika
kama akina Baba Yoyoo, hivi karibuni yalimkuta ya kumkuta baada ya
kukutwa akichafua mazingira maeneo ya Sinza Kijiweni, Kinondoni jijini
Dar, baada ya kutaitiwa na viongozi wa mtaa, OFM ilishuhudia.
Majira
ya saa 2.13 usiku, makamanda wa Kitengo Maalum cha Kufichua Maovu (OFM)
cha Global Publishers, wakiwa katika mizunguko yao ya kawaida,
walisikia vurumai zikitokea upande wa pili, na walipotupia macho,
waliona mkusanyiko ukiwa umemzunguka Mmasai huyo.
Baada
ya kusogea OFM ikaambiwa kuwa Baraka Mollel alikutwa akikojoa katika
mtaro wa maji machavu, kitendo ambacho ni kosa kwani anachafua
mazingira. Aliyeongoza ukamatwaji huo, alitajwa kwa jina moja la
Mubaraka aliyejitambulisha kuwa ni kiongozi wa mtaa huo.
Mmasai
huyo alitakiwa kulipa faini ya shilingi elfu 50, ambazo hakuwa nazo,
jambo lililomfanya ajitetee huku akilia na kuomba msamaha. Mmoja wa watu
waliokusanyika, alikuwa ni Mmasai aliyekataa kutaja jina lake,
aliyemtosa mwenzake kwa kumgongagonga na fimbo yake kichwani, akidai
ameidhalilisha jamii yao.
Hata
hivyo, kilio na maneno yake ya kuomba msamaha, yalisababisha baadhi ya
mashuhuda kuwasihi viongozi hao kumsamehe, wakisema kwake ni fundisho
ambalo pia wanapaswa kulipata watu wengine. Mollel alisamehewa na kupewa
onyo la kutorudia tena kitendo hicho katika eneo lolote jijini Dar es
Salaam.
Licha
ya Mmasai huyo, katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam, baadhi ya
wakazi wasio wazalendo, wamekuwa wakitupa mizigo ya takataka katikati
ya barabara nyakati za usiku na kusababisha usumbufu mkubwa wakati wa
mchana.
OFM
kinaungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye
amekuwa akisisitiza usafi na ulindwaji wa mazingira, kitu ambacho baadhi
ya wakazi wamekuwa hawakizingatii, hasa nyakati za usiku. OFM inaahidi
kutembelea na kupata picha za wachafuzi wa mazingira kote jijini Dar es
Salaam.
0 comments:
Post a Comment