Taasisi hiyo pia imekuwa ikijihusisha na mafunzo teknolojia ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa vikundi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuwafundisha juu ya utengenezaji wa matofali, vigae vya kuezekea nyumba pamoja na ujenzi wa nyumba za zenyewe ambapo taasisi na wananchi mbalimbali wanaweza kufaidika na mpango huo nchini.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na shughuli za kutengeneza vigae vya kuezekea nyumba katika karakana ya taasisi hiyo.
Balozi Ombeni Sefue akitembezwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiku Samson Mturi maeneo mbalimbali ili kujionea shughuli za zinazofanywa na taasisi hiyo.
Balozi Ombeni Sefue akiangalia wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati wakitengeneza vigae kwa ajili ya kuezekea nyumba.
Balozi Ombeni Sefue akipiga picha kwa simu yake huku wafanyakazi wa taasisi hiyo wakimuangalia baada ya moja ya nyumba ndogo iliyojengwa katika ghala ya taasisi hiyo kwa ajili ya mfano kumfurahisha.
0 comments:
Post a Comment