Stori: Dustan Shekidele, Risasi Jumamosi
MOROGORO:
Kijana aliyefahamika kwa jina la Kassim Said ‘Baunsa Rambo’ mkazi wa
jijini Dar ambaye inadaiwa ni mmoja wa mabaunsa wa Bendi ya Yamoto,
anasakwa na polisi kwa madai ya kuhusika na mauaji ya mchumba wake
aitwaye Mwajabu Ibrahim.
Tukio
hilo lilitokea Jumapili iliyopita ambapo inadaiwa kuwa, Kassim
alimshushia kipigo Mwajabu baada ya kutofautiana kabla ya kesho yake
mwanamke huyo kukutwa akiwa amekufa chumbani kwake.
“Hatukujua
kilichoendelea baada ya ugomvi ule mpaka kesho yake tulipopata taarifa
kuwa Mwajabu kakutwa amekufa. Kuna mwanaye anaitwa Fatuma, yeye atakuwa
na siri ya tukio hilo,” alisema mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya
jina lake.
Kufuatia
taarifa hiyo, mwandishi wetu alifunga safari hadi Mtaa wa Kilosa Town
Kata ya Mkwatani na kubahatika kuongea na mtoto wa marehemu
aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma Mayuwe ambaye alisema:
“Sasa sijui aliona nini kwenye simu, ghafla nikaona anampiga mpaka akatapika damu, watu wakawaamulia na hali ya amani ikarejea.
“Siku
chache baadaye kijana huyo ambaye ni Kassim alikuja na mshenga
kukamilisha taratibu zote za ndoa na tulichokuwa tunasubiri ni ndoa tu.
“Cha
kusikitisha ni kwamba juzi walipokuwa wanatoka kwenye Taarab zao,
kamfanyia ukatili na mwanangu amekufa. Taarifa zimefika polisi katika
Kituo cha Kilosa na bado anasakwa kwa mauaji hayo,” alisema mzee huyo
huku akilengwa na machozi.
Kufuatia
Kassim kudaiwa kuwa ni mmoja wa mabaunsa wa Bendi ya Yamoto, mwandishi
wetu aliwasiliana na Meneja wa bendi hiyo, Saidi Fella ambapo
alipoulizwa kama anamjua kijana huyo alisema:
“Huyo
baunsa siyo wa kwetu, hata mimi nimeshapigiwa sana simu kuhusu hilo
suala, sisi baunsa wetu anaitwa Mzungu, anakaa Temeke, huyo labda
atakuwa huwa anatumika kwenye shoo za bendi mbalimbali.”
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Ulrich Matei hakuweza kupatikana mara
moja kuzungumzia tukio hilo ila mmoja wa maafisa wa polisi aliyeomba
hifadhi ya jina lake alisema kuwa, Kassim anasakwa akihusishwa na mauaji
hayo.
0 comments:
Post a Comment