Rais
Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na vitendo vya rushwa
ambavyo vilinafanya jeshi hilo kukosa heshima katika jamii huku akisema
kuwa ana taarifa za jeshi hilo kuingia katika makubaliano ya kifisadi ya
mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kununua sare za jeshi hilo.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiwaapisha makamishna wa Jeshi
la Polisi waliopandishwa vyeo na kuongeza kuwa ni jambo la kusikitisha
kwamba mabilioni hayo yalitolewa kwa siku moja lakini hadi leo hakuna
hata sare moja ya iliyonuuliwa.
Ameshangazwa na jeshi hilo kutoa
kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa kati ya shilingi bilioni 40 hadi 60
kwa ajili ya sare za polisi ambazo hadi leo hakuna hata moja
iliyonunuliwa na wakati huohuo jeshi hilo likikosa shilingi bilioni 4 tu
za kukomboa magari yao zaidi ya 70 yanayoshikiliwa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) huko bandarini.
Aidha, Rais Magufuli ameagiza
uchunguzi ufanyike na wahusika wafikishwe mbele ya haki ila angalau hata
nusu ya fedha hizo ziweze kurudishwa zikalipie magari ya polisi yaweze
kutoka bandarini maramoja.
Amelitaka pia Jeshi la
Polisi kuachana na utaratibu wa kuwa na watumishi ambao ni raia wa
kawaida na badala yake polisi wenyewe ndio washike nafasi hizo kulingana
na taaluma husika na kushangazwa na taarifa kuwa Mhasibu Mkuu wa
Polisi aliyetumbuliwa hivi karibuni kwa tuhuma za ubadhirifu alikuwa
raia wa kawaida na sio polisi.

0 comments:
Post a Comment