Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) jana Jumatatu,
Julai 4, 2016 imezindua shindano la insha na maswali kuhusu Masoko ya
Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu Juu ya Tanzania
kwa mwaka 2016.
Akizungumza Jijini Dar es
Salaam jana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na
Dhamana (CMSA) Bibi Nasama M. Massinda alisema shindano hilo lina lengo
la kuongeza ueledi na ufahamu kuhusu masoko ya mitaji kwa wanavyuo hapa
nchini hali ambayo inatarajia kuchangia ongezeko la ushiriki wa
Watanzania kama wawekezaji, watoa dhamana na wataalum wa kutoa huduma
katika masoko ya mitaji pindi wanapohitimu masomo
yao.
‘Shindano hili lijulikano
kama Capital Markets University Challenge lina sehemu mbili – insha na
sehemu ya maswali kuhusu masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa vyuo na
taasisi za elimu ya juu, alisema Bi Massinda huku akiongeza kuwa
wanafunzi watapata fursa ya kuongeza elimu juu ya kuwekeza akiba kwa
njia endelevu na kuongeza matumizi ya Tehama kwa
wanavyuo.Wanavyuo watashiriki
Shindano la maswali na majibu kwa kutumia simu za kiganjani kwa kutuma
ujumbe mfupi wa maandishi kwenda namba 0766 046046, na kwa kutumia
tovuti na mtandao wa kompyuta. Kwa upande wa insha, wavyuo wanatikiwa
kuandika insha kuhusu fursa na faida za kutumia masoko ya mitaji katika
miradi ya maendeleo nchini.
Insha hiyo inatakiwa isizidi kurasa nne (4)
na kutuma kwa barua pepe kwenda "mail to:challenge@cmsa- tz.org" challenge@cmsa-tz.org.
Mshindi wa jumla katika kila shindano atapata zawadi ya 1,800,000/-
huku mshindi wa pili akipata 1,400,000/-. Pia washindi kutoka vyuo
vitatu bora – wavulana na wasichana, watapata fursa ya safari ya wiki
moja kutembelea makao ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana jijini
Dar es Salaam.Capital Markets
University Challenge ilizinduliwa mwaka jana ambapo liliendeshwa kwa
mafanikio makubwa na kuvuka lengo la ushiriki kwa zaidi ya 300%.
Mafanikio hayo yalitokana na jitihada za kuhamasisha matumizi ya
technolojia ya habari kwa matumizi ya simu za kiganjani, mtandao wa
kompyuta, barua pepe na wavuti, asema Bi Massinda huko akiongeza kuwa
mafanikio hayo yaliandika historia mpya katika sekta ya masoko ya mitaji
katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.Shindano ya Capital
Markets University Challenges ilizinduliwa tarehe 4 Julai 2016 na
likafika tamata Agosti 15, 2016.
0 comments:
Post a Comment