Wednesday, July 20, 2016



Katika kile kinachoonyesha kuwa hivi sasa hataki masihara,Kiongozi wa Upinzani Nchini Kenya Raila Odinga leo hii amezidi kumpa tumbo joto mtetea kiti cha Urais wa Kenya katika uchaguzi Ujao,Mhe Uhuru Kenyatta,ambapo leo Rail Odinga alijikuta akikumbana na wafuasi wengi kuliko ilivyo kawaida.

Raila ambaye ni kiongozi pia wa Muungano wa vyama unaojiita ODM leo walikusanya maelfu ya watu katika safari zao za kujiimarisha katika majimbo mbali mbali ya uchaguzi kabla ya kamoeni kuanza.

Inatarajiwa kuwa katika uchaguzi ujao wa Kenya,kutashuhudiwa upinzani mkali kutoka kwa Bwana Raila ambaye alishawahi kuwa Waziri Mkuu wa taifa hilo kwa wakati fulani.



0 comments:

Post a Comment