Stori: Mwandishi wetu , Risasi Jumamosi
GEITA:
Kimenuka! Katika gazeti damu moja na hili la Ijumaa Wikienda toleo la
Jumatatu iliyopita, ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa;
RAIS MAGUFULI; HUU NDIYO UNYAMA ALIOUFANYA MCHINA BILA KUFANYWA
CHOCHOTE, ishu ilimfikia Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na
amekinukisha.
Katika
habari hiyo, Mchina mmoja alitajwa kumtesa Mtanzania ambaye
hakujulikana jina mara moja kwa kumpa kipigo kwa madai kuwa, aliiba
madini kwenye Mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro mkoani hapa.
WIKIENDA KWA WAZIRI
Sasa,
baada ya gazeti hilo kutoka, waziri Nchemba alilisoma gazeti hilo
pendwa na kuamua kuchukua hatua baada ya kutoamini kuhusu ukatili huo na
hivyo kwenda eneo la tukio kujionea mwenyewe.
WAZIRI MGUU NA NJIA
Jumatano
iliyopita, waziri huyo alifunga safari hadi kwenye mgodi huo kwa ziara
ya kikazi lakini kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso ya kijana
huyo kutoka kwa raia wa China ambaye ni mmoja wa wamiliki wa mgodi.
KWANZA BAADA YA KUFIKA
Awali,
waziri Nchemba alijiridhisha kwamba, kulikuwepo na tukio hilo la Mbongo
huyo kuteswa na jamaa huyo wa Kichina kwa kumpa kipigo
kilichomsababishia kupoteza fahamu.
WAZIRI ALIJUAJE?
Waziri
Nchemba alilazimika kutinga mwenyewe ndani ya Gereza la Geita
alikoshikiliwa kijana huyo ikidaiwa kwamba, alishitakiwa na mwajiri wake
kwa kosa la wizi.
Katika
mahojiano na uongozi wa gereza hilo, Waziri Nchemba alibaini kuwa,
kijana huyo ndiye anayeonekana kwenye picha iliyosambaa mtandaoni kwa
uthibitisho wa makovu yaliyopo mwilini mwake na mavazi aliyovaa siku
anateswa na wakati yupo gerezani hapo.
WAZIRI, KIJANA HADI MGODINI
Katika
hali iliyoonesha kuwa, Waziri Nchemba ameamua kuwapigania Watanzania,
alimchukua kijana huyo na kwenda naye mgodini kwa ajili ya kuwatambua
waliomfanyia vitendo hivyo vya kinyama.
WAPO WABONGO
Katika
zoezi hilo, kijana huyo aliwabaini Watanzania watano ambao ni walinzi
wa mgodi huo na Mchina mmoja kwamba ndiyo walioshirikiana kumpiga hadi
kumjeruhi.
KIBAO CHAGEUKA
Kufuatia zoezi hilo la utambuzi, Nchemba aliagiza wahusika hao wakamatwe mara moja kwa hatua zaidi za kisheria.
MUHIMU KULIJUA HILI
Hata
hivyo, tukio la Mbongo huyo kuteswa si lile la kibarua mwingine wa
mgodi huo aliyejulikana kwa jina moja la Elisha, ambaye wiki iliyopita
alidaiwa kuanguka kisha kupoteza maisha akikimbizwa Hospitali ya Wilaya
ya Geita kwa matibabu ambapo kwenye mitandao ya kijamii, ilitumika picha
ya kijana aliyeteswa kuwa ndiye Elisha kabla ya kufariki dunia.
Kuhusu
tukio la Mbongo huyo kuteswa, katika toleo la Wikienda, Jumatatu
iliyopita, lilizungumza na msaidizi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Geita ambaye alikataa kutaja jina, yeye alisema kijana huyo kweli
aliteswa lakini alipaochiwa alirudi kwao, Bariadi, Shinyanga.
Alisema jeshi la polisi halikuchukua hatua yoyote baada ya mtendewa kutoripoti popote malalamiko ya kuteswa kwake.
GLOBAL YAPONGEZWA
Baadhi
ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers wameipongeza kampuni hiyo
wakidai kuwa, imekuwa ikiandika habari kwa kuchimba sana na nyingi
zimekuwa zikiwatatulia matatizo wananchi.
“Mimi
nilisoma ile habari ya kwenye Ijumaa Wikienda, nikasikitika sana. Sasa
nilipoona Waziri Nchemba amekwenda, nikajua amesoma gazeti. Kwa kweli
nawapongeza sana Global kwa kufichua maovu,” alisema Mwadamu Hassan,
mkazi wa mjini Geita.
0 comments:
Post a Comment