Mahakama mjini Kinshasa, imemuhukumu mwanamuziki Mkongwe Koffie Olomide kwenda jela miezi 18 kwa kosa la kumpiga mnenguaji wake/kudhalilisha utu wa Mwanamke.
Hukumu hiyo iliyotolewa juzi mjini humo, imemtaja mkongwe huyo kama sugu wa makosa hayo ambayo amekuwa akiyatenda mara kadhaa.
Msanii huyo ameanza kuitumikia adhabu yake katika gereza moja nchini humo, na wakati akiingia kwenye gereza hilo Koffie alisikika akisema hawapendi wanawake tena
Lazima wakukinai umewatumia vibaya mno kwa biashara, kuwanyanyasa nk. sio kwa upendo. Ukitoka huko utanyooka.
ReplyDelete