Wednesday, July 13, 2016

Huyu ndiye aliyewapiga risasi maafisa wa polisi watano nchini Marekani kabla yeye kupigwa rusasi na kuuawa.
Anaitwa Milcah Xavier Johnson(25) Alikuwa mwanajeshi wa Marekani aliyepelekwa Afghanstan!.

Alikuwa ni mmoja wa wadunguaji hatari kwenye vikosi vya jeshi la Marekani nchini Afghastani.
Baada ya kumuua , vikosi vya ulinzi vya Marekani vilifanya msako mkali nyumbani kwake na kukuta mabomu ya kutengeneza, silaha za kudungulia ( sniper rifles) , bullet proof jackets , kombati za kijeshi na vitabu mbalimbali vyenye kuonesha mafunzo ya kijeshi.
Wachunguzi hao wanasema Milcal alikuwa ni " lone shooter" kwenye mkasa huo. Hii ikionesha uwezo wa hali ya juu katika fani ya udunguaji ( sniping)

Alichokifanya Milcal ni kupanga silaha zake kwenye angle tofauti za jengo hilo kisha alikuwa akiwadungua askari hao kwa nyakati tofauti akihama toka angle moja kwenda nyingine kwa spidi kali ili kuwachanganya askari waliokuwa wakitafuta risasi zinatokea wapi.
Mkuu wa Polisi jimbo la Dallas Chief David Brown akiongea na waandishi wa habari alisema ; " ni shambulio lililopangwa vizuri sana kwa maana ya utekelezaji na baya kwa duru za kiusalama kwa jimbo letu na nchi yetu"
Habari kwa msaada wa mtandao wa CNN.

0 comments:

Post a Comment