TWIGA mwangavu aliyepewa jina la Omo ameonekana akivinjari katika
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire wilayani Monduli mkoani Arusha akiwa na
kundi la wenzake ambalo halikuonekana kumshangaa kutokana na
kutofautiana nao.
Mwanajiolojia Dk. Derek Lee, mwanzilishi na mwanasayansi katika
Taasisi ya Mazingira Asili, ndiye aliyembaini twiga huyo mwang’avu.
Derek(45), alisema: ‘Hali ya Omo kwa kitaalamu hujulikana kama
‘leucistic’, akimanisha sehemu kubwa ya seli za ngozi yake hazina uwezo
wa kutengeneza rangi lakini baadhi zina uwezo huo na ndiyo maana yu
mwangavu na macho mekundu au bluu kama walivyo binadamu albino.
“Hata hivyo twiga huyo si albino, bali kama tulivyoona ni leucism,
ambayo licha ya kuchangia macho mekundu au bluu kama albino, huwa na
ngozi nyeupe angavu wakati albino ni weupe kamili.
“Hii ni hali ya kinasaba,” ‘Omo ni twiga pekee mweupe ambaye hadi
sasa tunamfahamu, lakini tumewahi kuona wanyama wenye hali kama yake
wakiwamo kongoni, nyati na mbuni katika Hifadhi ya Tarangire’.
Aliongeza: ‘Omo anaonekana kuzoeana na twiga wengine, daima amekuwa
akionekana akiwa na kundi kubwa la twiga wa rangi ya kawaida ambalo
halionekani kujali utofauti wake wa rangi.
‘Omo kwa sasa ana umri wa miezi 15, akiwa amefanikiwa kupita mwaka
wake wa kwanza kama twiga mtoto kipindi ambacho ni hatari zaidi kwa
twiga wadogo kutokana kuwindwa mno na wanyama wakali wala nyama kama
vile simba, chui na fisi.
‘Fursa yake ya kuendelea kuishi ni kubwa lakini twiga wakubwa mara
kwa mara hukumbana na ujangili unaolenga nyama ya pori na rangi yake ya
ajabu inaweza kuwa kivutio zaidi kwa majangili.

0 comments:
Post a Comment