Khadija
Kopa amesema kinachosabisha wanawake kutosaidia wenyewe kwa wenyewe ni
‘nyodo’ ambapo amedai hata akienda hospitali ni bora atibiwe na daktari
wa kiume kuliko wa kike.
Akizungumza
katika kipindi cha Wanawake Live cha East Africa Television, Khadija
amesema wanawake wengi hawapendani wenyewe kwa wenyewe.
“Unajua
wanawake mara nyingi wananyodo hicho ndio kitu ambacho mimi mpaka leo
napenda kutibiwa na madaktari wanaume, yaani mimi sindano nataka
kuchomwa na mwanaume, hata kuzalishwa siku zote mimi nazalishwa na
madaktari wa kiume sababu wanawake hatupendani” alisema Khadja Kopa.
Lakini
mbali na hilo Malkia huyo wa mipasho aliwasii wanawake kupendana wao
kwa wao ili waweze kupiga hatua mbele zaidi na kusema kitendo cha
kutopendana kinawakwamisha kupiga hatua kimaendeleo na kujenga chuki
kati yao.
“Unajua
sisi wanawake hatupendani, mimi hapa ni mwanasiasa hivyo hata
nikigombea nafasi fulani nitapata kura nyingi zaidi kutoka kwa wanaume
na si wanawake, lakini ningependa leo niwaambie tu hata ukimkuta
mwanamke wenzako anagombea nafasi fulani muoneshe support ya moja kwa
moja, jamanii tunabidi tupendane” alisisitiza Khadja Kopa
0 comments:
Post a Comment