DODOMA: Huku
leo Rais Dk John Magufuli akitarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, viongozi na
makada wenye makandokando, maarufu kama majipu wamekaa mkao wa
kutumbuliwa wakati wowote.
Habari
kutoka kwa wajumbe ambao tayari wameshawasili mjini hapa, wanasema
baadhi ya viongozi ndani ya chama hicho wana kashfa ya kuhodhi ardhi na
mashamba kwa kutumia nafasi zao, kitu kinachowapa hofu kuwa mara tu
baada ya Magufuli kuchukua nafasi hiyo, watakuwa wa kwanza kuondolewa na
kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Ukiangalia
viongozi hawa wamekuwa wafujaji wakubwa wa mali za chama, miradi mingi
wameigeuza kuwa yao, wametumia ofisi za chama kupiga dili chafu, sasa
mtu kama Magufuli ambaye hataki mchezo na hacheki na watu
wajanjawajanja, wana hofu kubwa sana,” alisema mjumbe mmoja kutoka mikoa
ya Kaskazini.
“Baadhi
ya viongozi wa CCM wamefanya ubadhirifu mkubwa katika miradi ya chama,
wametumia maeneo yake kwa manufaa yao, utakuta ofisi imepangishwa
wafanyabiashara mbalimbali, lakini fedha hazieleweki zinakwenda wapi,
wakati mwingine wanafanya biashara zao kwenye majengo ya chama bila
kulipia kodi, kwa moto huu wa JPM, sidhani kama watapona hawa watu,”
alisema mjumbe mwingine wa Dodoma.
Mji
wa Dodoma umekuwa na wageni wengi wanaotokana na mkutano huo, wakiwemo
wajumbe, wageni waalikwa, watendaji wa taasisi mbalimbali za kitaifa
ambao wanahusika kwa namna moja au nyingine na mkutano huo ambao msingi
wake mkubwa ni kung’atuka kwa Mwenyekiti Kikwete na kukabidhiwa kwa
Magufuli.
0 comments:
Post a Comment