Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameipongeza benki ya Nmb kwa huduma Bora kwa wateja nchini na uchangiaji wa huduma za jamii ikiwemo elimu na Afya hapa nchini
Hayo ameyasema leo wakati hafla ya futari iliyoandaliwa na benki na benki ya NMB kwa wananchi mkoa wa Mbeya
Amesema benki ya Nmb imekuwa mstari wa Mbele katika uchangiaji wa madawati na sekta ya afya kwa mujibu wa taarifa benki imetumia shilingi bilioni 1.5 katika mambo ya kijamii
Amewashukuru Nmb kwa uamuzi wa kuwafuturisha wananchi Mkoa Mbeya na amewatakia mafanikio ktk shughuli za kibiashara na amewahamasisha wananchi kuitumia benki ya NMb
Aidha amewataka viongozi wa dini zote kushirikiana ili kudumisha amani na mshikamano



0 comments:
Post a Comment