Stori: Imelda Mtema, Wikienda
DAR ES SALAAM: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan amempongeza ‘kumpa tano’ Mtangazaji wa Kipindi cha Mboni Show kupitia TBC1, Mboni Masimba kwa kuwakusanya watoto yatima wa vituo mbalimbali jijini Dar kisha kuwafuturisha akimwambia kuwa amejumuika naye kwa roho safi aliyoionesha.
“Nampongeza sana Mboni ni wachache sana wanaoweza kujitoa kufanya jambo kwa ajili ya watoto yatima, Mboni ni mfano wa kuigwa,” alisema Mama Samia.
Mbali na Mama Samia, futari hiyo ilihudhuriwa na viongozi wengine kama Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, mabalozi wa nchi mbalimbali na baadhi ya mastaa wa Bongo.
0 comments:
Post a Comment