Na Mwandishi wetu, RISASI MCHANGANYIKO
DAR
ES SALAAM: Watu tisa wanaodaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja
(mashoga), wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni
wakituhumiwa kukusanyika kinyume cha sheria kwa lengo la kupinga amri ya
Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ya kupiga marufuku vitendo vya mapenzi ya
jinsia moja jijini hapa.Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini, watu hao walikamatwa baada ya polisi
kuvamia kwenye Ukumbi wa baa ya Matema uliopo Kinondoni B ambako zaidi
ya wanaume 200 wanaodaiwa kuwa mashoga, walikusanyika kwa lengo la
kujadiliana kwa kina kuhusu amri ya Makonda ya kuwapiga marufuku ili
kutoa tamko la pamoja.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake,
alienda kuonana na uongozi wa Ukumbi kwa maelezo kuwa wanauhitaji kwa
ajili ya kufanyia sherehe ya kuzaliwa (birthday) ya rafiki yao.
“Meneja
wa ukumbi alimhoji anategemea kuwa na wageni wangapi ili apime uwezo wa
ukumbi wake, akamjibu kwamba wanaweza kuwa kati ya 200 hadi 300, kwa
kuwa ukumbi ni mkubwa, walikubaliana ambapo mwanamke huyo alifanya
malipo kabisa,” kilisema chanzo chetu.
SIKU YA TUKIO ILIVYOKUWA
Siku
ya tukio, chanzo chetu kinasema meneja wa ukumbi, wahudumu na wateja
wengine waliokuwa wakiendelea kupata vinywaji, walishtushwa na kundi la
wanaume tata walioanza kuwasili ukumbini hapo kwa makundi.
“Walikuja
na magari ya kifahari, watu wakawa wanahisi huenda kuna kiongozi au mtu
maarufu anakuja, lakini tukawa tunashangaa wote wanaoshuka, wana dalili
za ushoga,” kilisema chanzo chetu na kuongeza kuwa, uongozi wa ukumbi
ulishindwa cha kufanya kwa sababu tayari ulishapokea fedha zote.
Inadaiwa
baada ya muda mfupi, eneo lote lilikuwa limefurika, wakaingia ukumbini
huku wengine wakiendelea kuwasili na wengine wakiwa kwenye magari
yaliyokuwa yamepaki nje ya ukumbi huo.
AJENDA YAO KUBWA
“Nasikia
ajenda yao kubwa ya kukutana, ilikuwa ni kupinga amri ya mkuu wa mkoa
ya kupiga marufuku mapenzi ya jinsia moja. Kabla ya siku hiyo, unaambiwa
tayari walishakuwa na vikao vidogovidogo katika maeneo mbalimbali ya
jiji na siku hiyo ndiyo walikubaliana kufanya kikao kikubwa ili kutoa
tamko rasmi,” kilisema chanzo chetu kilichoshuhudia tukio hilo mwanzo
mwisho.
Ni
wakati huo ndipo kamanda mmoja wa kitengo cha OFM (Operesheni Fichua
Maovu) cha Global Publishers alipotonywa, sambamba na askari Polisi
ambao walipowasili, walilizingira eneo hilo.
Askari
mmoja alimfuata meneja wa baa na kuzungumza naye, bila shaka akimhoji
juu ya kilichokuwa kinaendelea. Ghafla polisi wenye silaha wakivamia
eneo hilo na kuvunja kikao hicho pamoja na kuanza kuwakamata.
OFM
ilishuhudia purukushani kali ya aina yake baina ya wana usalama na
wanaume hao, lakini kwa kuwa watata hao walikuwa wengi, waliwazidi
ujanja na wengi wao kufanikiwa kukimbia.
Baada
ya kukamatwa, mmoja wa vijana hao anayedaiwa kuwa ni mtoto wa kigogo wa
Polisi, alimpigia simu baba yake ambae kupitia simu ya mtoto huyo,
aliomba kuongea na askari aliyeonekana kuwa kiongozi wa operesheni hiyo,
aliyejulikana kama Afande Makomeo ili aangalie jinsi ya kumsaidia mtoto
wake, lakini askari huyo alikataa akidai mbele yake kuna OFM huku pia
akisema mkuu wa mkoa ameshaambiwa idadi ya waliokamatwa.
OFM
iliwashuhudia vijana hao tisa wakipakizwa kwenye gari lililotumiwa na
Polisi, Toyota Noah lililokuwa na namba za usajili T980 CMQ na kupelekwa
katika kituo cha kidogo cha Polisi cha Mwinjuma, kabla ya baadaye
kuhamishiwa Oysterbay.
Katika
mtiti huo, inaelezwa kuwa meneja mkuu wa baa hiyo alitoweka akihofia
usalama wake kwani mashoga hao walikuwa wakimtuhumu kwamba ndiye
aliyewachoma kwa polisi.
Akizungumza
na gazeti hili kwa niaba ya meneja mkuu, John Magazini, ambaye ni
meneja burudani wa baa hiyo, alisema wakati wakichukua fedha za ukumbi
huo, hawakuelewa kama utatumiwa na mashoga.
Gazeti
hili lilimtafuta kwa simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,
Christopher Fuime, ambaye awali alipopokea na kusalimiwa, ikakatika.
Kuanzia wakati huo (saa saba mchana Jumatatu hadi saa kumi jioni) simu
yake haikuwa ikipatikana hewani ili kuzungumzia suala hilo
0 comments:
Post a Comment