Msanii
wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha tetesi za kwamba ana
bifu na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Dj Majay, Hamisa Mobeto.Lulu na MobetoMuigizaji
huyo ambaye kwa saa anadaiwa kutoka kimapenzi na Majay, aliingia kwenye
malumbano na baadhi ya mashabiki wa Mobeto katika mitandao ya kijamii
wakimtuhudi kuiba bwana.
Akiongea katika kipindi cha Weekend Chart
Show cha Clouds TV Ijumaa iliyopita, Lulu amesema hata tatizo na Mobeto
ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na Majay.
T“Sipendi sana kuongelea issue ambayo nitakuwa kama nachochea, mimi ni mtu fulani very peace, very very peace, sina tatizo naye,” alisema Lulu.
Akiongelea
kama ni kweli kuna watu walikuwa wanatumwa na Mobeto ili wamtukane
alisema “Siwezi kujua kwa sababu sijafuatwa direct, lakini sina tatizo
naye, mtu akinipa kijembe namchukulia kama mtu kanipa kijembe”
Hata
hivyo, Lulu na CEO wa EFM, Dj Majay kwa sasa wapo karibu zaidi, kwani
wawili hao wamekuwa wakipost picha zao katika mitandao ya kijamii wakiwa
pamoja.
By Yasin Ngitu

0 comments:
Post a Comment