MSANII
kutoka Bongo Muvi, Ester Kiama amesema anajutia kujiingiza katika fani
hiyo aliyoitamani muda mrefu baada ya kuona soko limeingia ‘mdudu’ mbaya
bora na kwamba bora angeendelea na biashara yake ya upambaji.
Akizungumza na Amani juzikati,
Ester alisema zamani alikuwa na shauku ya kutimiza ndoto yake ya kuwa
muigizaji mkubwa, lakini alipoanza kujulikana, soko la filamu limekuwa
gumu, haziuziki na hata msanii akipeleka kazi yake kwa wasambazaji,
malipo yake huchukua mwaka mzima.
“Najuta
bora hata ningeendelea na kazi yangu ya saluni na upambaji niliyokuwa
nikiifanya awali kuliko kujiingiza huku, soko hakuna. Unacheza filamu
unaiweka ndani tu utaipeleka wapi sasa, wanunuaji hawapo, inabidi wadau
wafanye kitu kurejesha soko,” alisema Ester.
0 comments:
Post a Comment