Stori: Imelda Mtema
HUKU
kukiwa na madai ya kuporomoka kwa soko la filamu nchini, muigizaji
mahiri Yusuf Mlela amekiri kuwa licha ya kufanya kazi nyingi, lakini
hakuna chochote cha maana alichopata katika maisha yake ya uigizaji.
Akizungumza na Risasi Vibes, Mlela
alisema katika kuhakikisha anasonga mbele, nusu ya maisha yake
ameyahamishia jijini Nairobi, nchini Kenya ambapo angalau anaona mambo
yake yanaweza kwenda vizuri.
“Unajua
kiukweli nimeuza sura sana kwenye filamu nyingi lakini mafanikio ni
kiduchu mno, sasa nimeamua kutafuta njia nyingine ya kuweza kunisogeza
hatua moja kimaisha, niko Nairobi na huko nafanya tamthiliya, nahisi
mambo yataenda vizuri,” alisema Mlela.
0 comments:
Post a Comment