Maafisa
wa upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa programu ya komputa
inayotumiwa na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton
imedukuliwa.Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa
wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta hiyo.Awali kamati
ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa
mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.Vyombo vya habari Marekani
vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za
Urusi.
Shirika
la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa linaendelea na
uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha udukuzi huo dhidi
ya kompyuta za chama cha Democratic.Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.
0 comments:
Post a Comment