Friday, July 29, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Manyoni Mkoani Singida mara baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo akiwa njiani kuelekea mkoani Singida. 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wakazi wa Singida mara baada ya kuwasili. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wakazi wa Manyoni mara baada ya kumaliza kuhutubia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
Mbunge wa manyoni Magharibi Yahya Masare akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za asili cha Manyoni kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli kuhutubia mkutano katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ikungi waliomsimamisha wakati akielekea Mkoani Singida. PICHA NA IKULU

1 comment:

  1. Mbowe na yeye ni mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, kama Magufuli alivyo mwenyekiti wa chama chake. Iweje yeye aende Singida AENDE basi aende huko kwao chato usiku navmchana

    ReplyDelete