Na Andrew Carlos
AMEVUNA
alichopanda! Unaweza sema hivyo kwa maana nyingine baada ya wikiendi
iliyopita ndani ya Kenya kutawala kwa sakata jingine la mwanamuziki
mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Koffi Olomide
la kumshambulia dansa wake wa kike aliyejulikana kama Pamela.
Koffi
a.k.a Le Grand Mopao amekuwa na matukio yanayomuweka hatiani na hili
alilolifanya la kutimuliwa nchini Kenya limedhihirisha kuwa amevuna
alichopanda.Ikumbukwe kuwa mwaka 2012, staa huyo aliwekwa jela miezi
mitatu nchini mwao kwa kosa la kumshambulia prodyuza wake, Diego Lubaki
baada ya kuombwa kulipwa pesa ya kutengeneza video.Pia mwaka huohuo
akiwa Paris, Ufaransa Koffi alifunguliwa mashtaka na madansa wake watatu
baada ya kudaiwa kuwabaka na kuwafungukia ndani kinyume cha sheria.
La Kenya ilikuwaje?Koffi
alialikwa kufanya shoo siku ya Jumamosi (wikiendi iliyopita) nchini
Kenya katika Ukumbi wa Bomas na ilipofika Ijumaa alikuwa amewasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Akiwa
ameambatana na madansa wake wa kike kama ilivyo ada ya waandishi,
alifanyiwa mahojiano na moja ya TV nchini humo (Citizen) na akiwa
katikati ya mahojiano hayo alisikia ugomvi nyuma yake baina ya madansa
wake ndipo alipoachana na mahojiano na kumvamia mmoja wa madansa wake
(Pamela) na kumpiga mateke hadi pale alipoamuliwa na maafisa wa polisi
wa uwanja huo.
Wakenya wacharuka
Baada
ya kipande cha video kusambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha
udhalilishaji huo. Wakenya kwa ujumla waliungana na kukemea kitendo cha
staa huyo anayebamba na Wimbo wa Selfie kuwa atimuliwe nchini humo,
hafai na ameonesha kuwadhalilisha wanawake. Wakenya hao waliungana kwa
kukataa msanii huyo kufanya shoo nchini humo na akamatwe mara moja kwa
kuweka Hash Tag (KickKoffiOlomideBackToCongo) kwenye mtandao wa Twitter.
Ajitetea
Koffi
alijitetea kuwa hakukusudia kumsha-mbulia Pamela na kwamba kwanza
aliona kama dansa huyo alitaka kuibiwa pochi hivyo alienda kuamulia.
Pili anasema alikuwa anajaribu kumtetea kwani mmoja wa maafisa wa kike
katika uwanja huo wa ndege alikuwa akiwasumbua madansa wake.
Atimuliwa
Baada
ya taarifa kusambaa, mkuu wa polisi nchini, Kenya Joseph Boinnet alitoa
taarifa na kuwaagiza polisi wachukue hatua ambapo Ijumaa usiku
alifukuzwa kwa kusafirishwa na Shirika la Ndege la Kenya Airways kwenda
kwao, Kinshasa.
Wakenya wameonesha mfano
Wakenya
wameonesha mfano wa kuigwa hata nchini kwetu kwa kuungana pamoja na
kukemea unyanyasaji wa wanawake. Wameonesha kuwa ukatili kwa wanawake
hautakiwi katika jamii na siyo kwa wanawake wa nchi yao bali kote
duniani kwani dansa aliyepigwa na Koffi hakuwa Mkenya bali ni Mkongo.
Ameleta hasara kubwa
Kwa
alichokifanya Koffi, kwanza ameingiza hasara kubwa kwa promota
aliyeandaa shoo hiyo, pia amepoteza muda na kiasi kikubwa cha pesa
kuanzia gharama ya hoteli, ukumbi, usafiri na vingine vingi.
0 comments:
Post a Comment