Friday, July 8, 2016

​Ciara na mchumba wake, mchezaji wa Seattle Seahawks, Russell Wilson wamefunga ndoa.
Wawili hao wamefunga ndoa Jumatano hii,
mjini Liverpool,  Uingereza. Kwa mujibu wa TMZ ndoa yao imehudhuriwa na watu takriban 100 ambao ni ndugu wa karibu ma marafiki zao.
Bibi harusi alikuwa amevaa shela maalum ya Roberto Cavalli.
Ciara ameshare picha kwenye Instagram akiwa na mume wake na kuandika: We are The Wilsons!”
Jennifer Hudson, Kelly Rowland, La La Anthony walikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria harusi hiyo.
Wawili hao walichumbiana mwezi March baada ya kuanza kuwa pamoja April 2015 kufuatia kuvunjika kwa uhusiano wa Ciara na Future.

0 comments:

Post a Comment