
Davis Mosha akisalimiana na watoto wakati wa futari
|
Mfungo wa mwezi wa Ramadhani ni nguzo ya nne ya dini yetu ya kiislam katika nguzo tano. Imefaradhishwa funga hii ndani ya mwezi wa Sha,abani mwaka wa pili tokea Bwana Mtume (S. A. W) kuhamia Madina, akafunga Bwana Mtume (S. A. W) katika maisha yake alifunga ramadhani tisa
Amesema
Bwana Mtume (S. A. W) “Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa
kuonekana mwezi na kama pakiwa na mawingu basi kamilisheni siku
thelathini”
Watoto wakipata futari
|
Maneno haya ya Bwana Mtume (S. A. W) yanathibitisha yale tuliyotangulia kuyasema juu ya kuthibitika kwa kuingia mwezi wa Ramadhani na kuanza kwa funga ya ramadhani. Lakini njia nyingine inayokubalika ni uthibitisho wa kusikia kutoka kwa Yule atakaekuja na taarifa ya kuwa ameuona mwezi na akawa ni miongoni mwa waislamu. Njia hii inakubalika kuwa ni miongoni mwa waislamu. Njia hii inakubalika kuwa ni dalili kamili na inayojitosheleza kuwa tayari mwezi umeandama na funga ya ramadhani imeanza.
watoto wakifurahia futari
|
Leo ikiwa ni siku ya 27 toka waumini wa dini ya Kiislam kuanza kufunga baada ya Mwezi kuandama. Katika Kipindi cha Mfungo wa Ramadhan tamaduni za waislam hukusanyika na kufuturu pamoja huku mahitaji muhimu ya makundi mbalimbali ya kijamii yakitolewa katika kipindi hiki kama moja ya kutoa sadaka kwa jamii.
Leo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro Mfanyabiashara Mkubwa Tanzania ndugu Davis Mosha amefuturu pamoja wa watoto yatima wa Manispaa ya Moshi. Davis Imekua kawaida yake kila kipindi cha mfungo huweza kukutana na watoto yatima na wasiojiweza na kufuturu nao huku akisikiliza matatizo yao na kuyatatua.
Davis Mosha akipata futari na watoto
|
Akizungumza katika Hafla hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Bakwata Mkoa wa Kilimanjaro Davis Mosha alisema huu ni wakati wa kusaidia watoto hawa wenye mahitaji maalum. "Nimedhamiria kuwasaidia watoto hawa na nimewasikiliza wanahitaji kusaidiwa, Viongozi wa hivi vituo waorodheshe mhitaji yao na nitawasaidia, Ni lazima wasome na watimize malengo yao, Ni lazima wajihisi wapo na wazazi wao." Alisema Davis Mosha.
Davis Mosha akizungumza na watoto
|
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Vituo Ndugu Lukanga alisema watoto wamefarijika sana na wamejivunia wamefurahia sana na watoto wanamuombea kwa Mungu aendelee kuwa na Moyo huo huo.
0 comments:
Post a Comment