Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.
Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.
Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.
Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment