Ukitaka
kunijulia hali, mimi sijambo. Ni mzima wa afya. Naendelea kupambana
ndani ya mjengo huu mkubwa wa magazeti Pendwa, Global Publishers. Hapa
sisi ni kazi tu. Kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha jamii yetu.
Madhumuni
ya kukuandikia barua hii kwanza kabisa ni kukupongeza. Kwa kila mwenye
akili timamu yenye kuwaza kwa mlengo chanya wa Muziki wa Bongo Fleva,
kamwe hawezi kuacha kupongeza kazi nzuri uliyoifanya na wale mapacha
kutoka Nigeria, P-Square.
Umewakimbiza.
Umeonesha unajua kuimba na kucheza zaidi yao. Harakati zako
unazozifanya kila siku katika kuhakisha unapiga hatua wewe binafsi na
Bongo Fleva kwa ujumla ni mpuuzi pekee anayeweza kukupinga na kusema
labda hufai.
Unajua
kuandaa muziki na kuuachia kwa wakati. Una timu nzuri ambayo inakujenga
kistaa kwa kufuata au kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali
waliofanikiwa kimuziki. Ninapokupongeza kuhusu suala la kujifunza kutoka
kwa waliokutangulia, hapo pia kuna msingi wa barua yangu.
Niwe
mkweli ndugu yangu, sijafurahishwa na namna ambavyo ulijirekodi video
zenye mlengo wa kujidhalilisha ili tu kutengeneza ‘awareness’ ya wimbo
wako. Ukaamua kuingia bafuni, wewe na mpenzi wako mkayafanya yale
mliyoyafanya.
Binafsi
najua hata yale uliyoyafanya, umeiga. Yawezekana ni wewe au uongozi
wako ulikupanga wewe kufanya vile ili kutengeneza ile kiki lakini kitu
cha msingi ninachotaka kukuambia, lazima utambue utamaduni wetu pia.
Kuna
kiki nyingine haziendani na utamaduni wetu. Masuala ya kuonesha mambo
mliyoyafanya faragha, kwa mila na destuli zetu za Kitanzania,
haipendezi. Watanzania wanajua kuiheshimu faragha. Mbona kuna vitu vingi
unaweza kufanya na vikatengeneza kiki?
Bahati
nzuri wewe watu wanakuelewa. Hauhitaji kufanya vitu vya kujidhalilisha
saana ili waweze kukuzungumza. Yale mambo ya wewe kumlamba mpenzi wako
kwapani huku unakula, siyo ishu. Watu wengi wanayafanya tena pengine
zaidi ya yale lakini kamwe hawawezi kuyaweka kwenye mitandao.
Kwanza
ni kujidhalilisha, pili ni kujishushia heshima wewe na huyo mpenzi
wako. Watu wanaojua zaidi ya ulivyofanya pia wanaweza kukucheka na
kukuona pengine hujui. Au wanaweza kusema wewe mshamba wakati wewe si
mshamba. Una maana yako.
Maana
yako ifanye katika njia ambazo haziwezi kuharibu Utanzania wako. Wewe
una watu wanakuheshimu. Una wazazi, una jamii kubwa tu inayokuheshimu
wakiwemo hata viongozi wa kiserikali, unapofanya mambo ya aina hiyo
yanaweza kukukosesha hata baadhi ya michongo ya kazi.
Ni matumaini yangu utakuwa umenielewa na utaufanyia kazi ushauri wangu. Nakupongeza na pia nakuomba ubadilike.
Mimi ni ndugu yako;
0 comments:
Post a Comment