EMMANUEL
Elibariki ndilo jina lake halisi, lakini amejipatia umaarufu mkubwa kwa
jina la Nay wa Mitego katika Muziki wa Bongo Fleva. Unapozungumzia
marapa vijana waliochipukia baada ya wakongwe kina Sugu, Prof Jay, Fid
Q, AY, FA na wenzao wa kizazi hicho, huwezi kumuweka kando dogo huyu.Ninasikiliza
mara nyingi kazi zake na mojawapo iliyonikaa ni ile aliyofanya kolabo
na Diamond ya Muziki Gani. Ukiisikiliza ile ngoma, ndipo unatambua jinsi
gani rap na uimbaji unaweza kuleta kitu tofauti ukichanganywa. Lakini
zaidi kilichonivutia, ni ule ukweli wa mipasho waliyokuwa
wakibadilishana na Diamond.
Moja
ya vitu vikubwa vinavyombeba Nay ni sauti yake nene na jinsi
anavyotambaa kwenye midundo ya muziki wake, ni jambo lingine
linalokufanya uvutiwe naye. Ni mtu anayekufanya usione pengo
linaloonekana kuwepo la kukosekana kwa Chid Benz katika ubora
uliotukuka.
Ukweli wa Hip Hop
Ninafahamu,
Hip Hop ni aina ya sanaa ya tambo, yenye kuakisi ukweli wa maisha ya
jamii. Ndiyo maana nchini Marekani, wengi waliofanya Hip Hop ni kama
wanaharakati wa kutetea haki ya watu weusi, ambayo walikuwa wakiielezea
kwenye nyimbo na video zao, kama jinsi wanavyobaguliwa, kuteswa au
kudhalilishwa na weupe, achilia mbali pia kuwa waliitumia kutamba,
kuonesha ufahari wao katika mambo mbalimbali.
Marapa
wa Bongo niliowataja pale mwanzo, walifanya hivyo pia na kujizolea
umaarufu mkubwa, kwa kuwa walizungumza mambo yenye kuakisi maisha halisi
ya jamii yao.
Anapokosea Nay
Ukichunguza
sana nyimbo za Nay, unagundua kuwa licha ya kutembea kwenye Hip Hop kwa
maana ya tambo, lakini ana ukweli uliopitiliza ambao maadili ya jamii
iliyomkuza yanamkataza.
Katika
ngoma yake ya Nasema Nao, kuna mistari inayowa-dhalilisha akina dada wa
Bongo Muvi pia katika Ngoma ya Shika Adabu Yako, pia ametoa kashfa za
kutosha tu kwa wenzake hadi wengine kuwadhalilisha.
Na
mara zote hizo, wadau wakiwemo Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),
wamekuwa wakimpigia kelele kiasi cha kufikia hata ngoma yake ya Shika
Adamu Yako kufungiwa. Lakini kana kwamba haitoshi, hivi karibuni msanii
huyu ameachia ngoma nyingine, Pale Kati Patamu, dah! Haifai.
Nimetazama
‘clip’ ndogo ya video ya ngoma hiyo, kwa kweli haufai. Huu unawafaa
zaidi akina P Diddy ambao hata asili yao hawaijui.
Ushauri kwa Nay
Nimshauri
Nay, yeye bado bwana mdogo sana kwenye huu muziki, ana kipaji kizuri tu
na tena nje ya jukwaa, ana nidhamu ya kutosha. Aaachane na aina hii ya
Hip Hop, itamuondoa sokoni na wanaokashifiwa au kudhalilishwa na
mashairi yake wanaweza kumpeleka jela.
Maisha
ya usela yana muda wake na unapofikia hatua ya kumiliki hela za
kutosha, jina kubwa na hadhi, unahitaji nini tena zaidi ya heshima? Huu
ni wakati wa Basata kuonesha makucha, siyo tu kumsh-ikisha adabu Nay,
bali pia studio zinazote-ngeneza nyimbo na video zake!
0 comments:
Post a Comment