DAR
ES SALAAM: Ubuyu wa motomoto wa mjini ni kwamba, zile mbwembwe zote za
penzi la mastaa wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Idris Sultan,
zinadaiwa kufikia ukingoni na sasa imebaki stori kwani Wema, Idris
wamwagana rasmi.
Wikienda limeng’atwa sikio kuwa,
kitendo cha wawili hao ‘kushoo lavu’ kwenye ile Pati ya Black Tie
iliyofanyika juzikati katika Ukumbi wa King Solomoni pale Namanga, Dar
ilikuwa ni geresha tupu kwani walishamwagana kitambo.
Hata
hivyo, kama utakumbuka au hukuipata ni kwamba iliwahi kuvujishwa kwenye
mitandao ya kijamii kuwa Wema na Idris wamemwagana lakini baadaye
zilivunjwa picha zikiwaonesha wakiwa wameshikana mikono na mahaba tele
ili kuua soo.
wema-na-idriss-insta Sasa ubuyu
ulionyooka kutoka kwa chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa
mastaa hao unadai kwamba, kilichotokea kwenye pati hiyo zilikuwa ni
mbwembe za kuzuga zilizotokana na huruma ya Idris.
Ilidaiwa
kwamba, Idris alilazimika kufika kwenye sherehe hiyo kwa sababu
ilishatangazwa kuwa atakuwa ni miongoni mwa ‘ma-hosti’ lakini ukweli ni
kwamba mambo yalishaharibika.
wema na idris 2“Unajua
watu wengi hawakujua kuwa Wema na Idris walishaachana kitambo na pale
(King Solomoni) walikuwa wanafanya maigizo tu, japokuwa haijulikani moja
kwa moja sababu ya kuachana kwao lakini Wema anadaiwa kuwa tatizo kwa
Idris kutokana na kutokea kwa migogoro ya kila kukicha,” alitonya sosi
huyo.
Hata hivyo, katika kuonesha kwamba kuna kitu
kinaendelea, wana-ubuyu wetu walifuatilia akaunti zote za mastaa hao
katika mitandao ya kijamii kuona kama mbwembwe zao zinaendelea na
kubaini kuwa hawako sawa baada ya kusoma ujumbe wa Wema unaoonesha
kumbembeleza Idris huku jamaa huyo akionesha wazi kuwa hakuna mapenzi
bali ni drama tu.
Ili kuleta ushahidi, tunakukaribisha hapa kusoma nukuu zao mtandaoni;
MANENO YA WEMA
“Having
you as a friend, a brother, a lover and of course a shoulder to cry on
every time, i’m at my worst has been the best feeling ever… I wouldn’t
want to lose this feeling over anything…
“I realized without u
then i ain’t complete…. You have stood by me in good times and bad and
even when i messed up so bad you would look me in the eyes and tell me,
“Baby, its okay, we gona fix this”…
“Idris you have been one of a
kind and losing u is the last thing i want on this earth… I will love
you until forever, until death do us part we will be together…
“I
will hold on to you till da last minute because together we will get
there…. I love you with my life…. For I believe you are my true love, my
baby and inshallah! The Man that my kids will call daddy…” alimalizia
kuandika Wema akimlilia Idris.
IDRIS NAYE ALIANDIKA:
“Kumbuka kurekebisha kiatu kila hatua ya maisha unayopiga kisije kuchomoka ukakanyaga mwiba ukapunguza spidi.”
WEMA ASAKWA
Wikienda
halikuishia hapo kwani lilimsaka Wema anayedaiwa kubwagwa, alipopigiwa
simu hakupokea, akaandikiwa ujumbe mfupi wa sms ambao pia hakuujibu.
Pia alitumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp lakini pia hakujibu.
UBUYU WAKAMILIKA KWA IDRIS MWENYEWE
Wikienda liligeuza dira yake na kuielekeza kwa Idris ambaye alifunguka bila kuacha lolote.
Kwa
mujibu wa Idris, yeye na Wema walishasahau kuwa waliwahi kuwa na
uhusiano wa kimapenzi kwani kwa sasa kila mtu ana ‘biashara’ zake.
“Mimi
nilikwenda kwenye ile pati kwa sababu ya kuwaonea huruma tu kwani ndiyo
kwanza wameanzisha kampuni na mbaya zaidi walikuwa wakiniweka kwenye
matangazo. Unadhani watu wangewachukuliaje? Sikutaka kuwaharibia shoo
lakini mimi nilishaachana naye na nina biashara zangu nyingine,”
alifunguka Idris.
Idris alienda mbali zaidi na kusema
kuwa kwa sasa ana mwanamke mwingine anayempenda na siku si nyingi mambo
yakikaa sawa, atamuanika.
“Mwenzenu nina kifaa kingine soon nitawafahamisha,” alisema Idris.
WEMA NA IDRIS
Awali
Wema na Idris walificha uhusiano wao lakini baadaye waliamua kujiachia
ambapo mlimbwende huyo alidai kushika ujauzito lakini kwa bahati mbaya
ukachoropoka.
Source:Global Publishers

0 comments:
Post a Comment