
Mashindano ya Qur'an kwa watu mashuhuri, siku ya kesho kuanzia saa nne kamili asubuhi mpaka 10 alasiri kutakuwa na mashindano na usomaji wa Qur'an kwa watu mashuhuri katika ukumbi wa KING SOLOMON ambapo lengo kubwa ni kuhamasisha watoto kujali swala zima la madrasa na usomaji Qur'an na hata wazazi kutosahau kuwapa watoto wao elimu ya dini pia, kupitia watu mashuhuri rofauti watakaosoma itamfanya mtoto aone faida na umuhimu wa kuhifadhi Qur'an.. mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhwani KIKWETE ambae nae atasoma pia, lakini kutakuwa na watu wengine tofauti kama HARMONIZE, ALI KIBA, GABO, SUMALEE, WEMA SEPETU, DAHUU, MASOUD KIPANYA, ABDU KIBA, ZAMARADI MKETEMA, BABU TALE, MADEE, QUEEN DARLENE, MWASITI ALMASI na wengine wengi ambao nao watasoma pia.. kiingilio ni BURE kabisa.. tukutane kwa ajili ya kuusindikiza mwezi wetu mtukufu kwa kusoma Qur'an kwa pamoja, WOTE MNAKARIBISHWA!!
0 comments:
Post a Comment