FUNCHAL, Ureno
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo hatimaye ameifungua hoteli yake ya nyota tano ambayo inaonekana kuwa na ubora wa kiwango cha juu hasa katika suala la ubunifu wa majengo.
Ronaldo ambaye kwa sasa yupo katika mapumziko kwenye Fukwe za Ibiza, Hispania amekamilisha mradi huo wa hoteli ambayo ipo katika Mji wa Madeira ambako ndipo nyumbani kwao.
Hoteli hiyo iliyopewa jina la The Pestana CR7 Hotel, ina vyumba 48 vya kulala, gym na bwawa la kuogelea ni moja ya hoteli nne ambazo mchezaji huyo amepanga kujenga.
Gharama ya kulala katika hoteli hiyo kwa usiku mmoja ni pauni 180 (Sh laki 5), kuna huduma ya bure ya internet, pia kuna baadhi ya vyumba ambavyo kutokana na ubora wake kulala kwa usiku mmoja ni pauni 575 (Sh milioni 1.6).
Hoteli nyingine ya Ronaldo ambayo inatarajiwa kufunguliwa baadaye mwaka huu itapatikana Lisbon, Ureno nyingine zitafunguliwa Madrid, Hispania na New York, Marekani.
0 comments:
Post a Comment