Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewataka madiwani wa halmashauri zote saba Mkoa wa Mbeya kutenga na kusimamia upelekaji Fedha kwa vikundi vya Vijana na wanawake kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na serikali
Hayo ameyasema Leo wakati wa kikao na madiwani wa halmashauri ya Mbeya Dc wakati wa kujadili hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali

Amewaambia halmashauri zinatenga Fedha asilimia 10 katika bajeti zao kwa ajili ya kusaidia vikundi vya Vijana na wanawake lakini inapokuja katika utekelezaji Fedha hizo hazipelekwi 

Hivyo amewataka halmashauri zote kutenga na kuzifuatilia Fedha hizo ziende kwenye vikundi na vikundi vitakavyopata hizo Fedha hizo vielezwe umuhimu wa urejeshaji wa fedha hizo kwa riba nafuu



0 comments:
Post a Comment