Tuesday, July 12, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya leo amekutana na wafanyakazi, menejimenti ya kiwanda na Kamati ya watalaam masuala ya kazi na Kamati ya Ulinzi na usalama kumaliza mgogoro wa wafanyakazi waliokuwa wakidai kucheleweshewa mishahara,kutowasilisha michango ya NSSF na kuboresha mazingira ya kazi na mikataba ya ajira
Ameagiza menejimenti kulipa mishahara ya miezi miwili ndani ya wiki mbili jambo ambalo uongozi umekubali kutekeleza
Kuhusu malimbikizo ya michango ya Nssf kwa kiasi kikubwa karibia malimbikizo yameshalipwa
Ameagiza Chama cha wafanyakazi kukaa na menejimenti haraka kuandaa mkataba ambao ndani yake utagusia mambo muhimu ikiwemo maslahi ya wafanyakazi,matibabu, usalama kazini na maslahi mengine Muhimu wafanyakazi
Amewataka wafanyakazi nao kushirikiana na uongozi na kutimiza wajibu wao kwa kufanya hivyo wataongeza tija na ufanisi kwani haki inaendana na wajibu 

0 comments:

Post a Comment