Tuesday, July 12, 2016

Wakuu wa mikoa ya Mbeya , Iringa,Njombe na wadau mbalimbali wamekutana jijini Mbeya kujadili namna bora ya kutatua mgogoro kati ya hifadhi ya Ruaha na wananchi wa vijiji 34
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa mitatu mwenyekiti wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amekiri kuwepo kwa mgogoro huo uliodumu kwa miaka mingi na sasa ni muda muafaka wa kumaliza mgogoro huo
Katika kushughulikia jambo hili Tanapa wamehaidi ifikapo August mwezi ujao watalipa wananchi waliopisha hifadhi mapunjo ya fidia sh milioni 362 . Fedha hizi ni kwa ajili ya wananchi waliolipwa fidia awali
Amesema kila mwananchi atapata haki yake kwa mujibu wa sheria na ameagiza ofisi ya CAG kukamilisha uchunguzi wa malipo ya awali ya fidia
Aidha watawashirikisha wananchi kila hatua katika kutatua mgogoro huo kwa kukaa na wananchi kwenye maeneo yao

0 comments:

Post a Comment