Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema mazingira ya kisiasa na kijamii yaliyopo nchini sasa ni mazuri kuliko kipindi chochote nyuma kwa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF) kufanikisha kampeni yake ya muda mrefu ya kuondoa sheria zote kandamizi kwa wanawake katika masuala ya mirathi.
Akiongea na viongozi wa WILDAF wakiongozwa na mpigania haki za akina mama na mwanasiasa mkongwe nchini, Bi.Tabitha Siwale jijini Dar es Salaam leo, Dk. Mwakyembe amesema WILDAF washindwe wenyewe kwani kuna mabadiliko chanya makubwa nchini ya fikra kuhusu haki za akina mama.
Waziri Mwakyembe amewahimiza WILDAF kupeleka mapendekezo ya mabadiliko ya sheria mbalimbali hasa zile za mirathi wizarani mapema iwezekanavyo ili kazi ya kuondoa mapungufu kwenye sheria hizo ikamilishwe.
0 comments:
Post a Comment