Na RICHARD BUKOS,
DAR
ES SALAAM: Lile gari la kifahari aina ya Range Rover Evogue lenye namba
za usajili AEK 101MP la muigizaji Wema Sepetu ‘Madam’, limewekwa kiporo
na madalali wa Yono Auction Mart waliokuwa wakiyapiga bei magari
yaliyokamatwa kwa makosa mbalimbali na wenyewe kushindwa kuyakomboa.
Gari
hilo lenye thamani ya shilingi milioni 200 lilikamatwa maeneo ya
Mbezi-Africana jijini Dar likiwa na msala wa kuingizwa nchini kinyume na
utaratibu sambamba na kutolipiwa kodi.
Jumatatu
iliyopita, paparazi wetu aliyekuwa na taarifa za mnada huo, aliibuka
kwenye yadi ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) iliyopo nyuma ya Jengo la
Water Front jijini Dar ambapo ilipotimu saa tano na nusu asubuhi, mnada
ulianza rasmi.
Kabla
ya kuanza mnada huo matajiri zaidi ya hamsini walianza kuyakagua magari
yaliyopo kwenye yadi hiyo ingawa mengi yaliyopigwa mnada yalikuwa
katika yadi zingine ikiwemo ile ya Baridi, Mnazi Mmoja.
Baadhi
ya matajiri walionekana kulitolea macho gari la Wema huku wengine
wakisema kutokana na kukaa yadi kwa takriban mwaka mmoja na kupigwa mvua
na jua hadi kufikia kuota majani, linaweza kuwasumbua.
“Hapa
tuna utaratibu wetu kwa kupiga mnada magari kwa awamu, lakini hata
hivyo mimi siyo msemaji wa ofisi, hebu nenda kamuone ‘inchaji’ wa ofisi
hii yule paleee… anayeonekana kwenye kioo yule, kata pale kulia halafu
pinda kushoto kaongee naye japo sasa hivi namuona ana wageni,” alisema
mfanyakazi huyo.
Paparazi
wetu alikwenda kwenye ofisi hiyo na kukaa kwenye foleni ya kumuona
inchaji huyo na ilipofika zamu yake, bosi huyo alimwambia amsubiri
mapokezi mpaka atakapomuita, jambo ambalo halikufanyika.
Katika
mnada huo, magari zaidi ya hamsini yalipigwa mnada ambapo gari aina ya
Toyota Vitz yaliuzwa kati ya shilingi milioni 5 na kuendelea, Toyota
Coaster (shilingi milioni 40), Toyota Prado (shilingi milioni 17), Benzi
(shilingi milioni 20), Toyota Swift (shilingi milioni 5), vichwa vya
Skania milioni 40 lakini vyote viliwahiwa na matajiri kabla wengine
hawajapanda dau.
0 comments:
Post a Comment