DAR
ES SALA-AM: Ule uhusiano uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano
unaowahusisha wasanii wanaotamba katika Muziki wa Bongo Fleva wakitumia
jina la Navy Kenzo, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ pamoja na Aika Mareale
unadaiwa kutibuka huku sababu ikimuhusisha msanii wao anayejulikana kama
Rosa Ree.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo cha karibu na wasanii hao wanaotamba na vibao vingi
ikiwemo Aiyola, Game, Kamatia Chini na vingine kibao, kwa sasa wamekuwa
kama chui na paka na wapo katika kujutia kwa kumuweka Rosa katika lebo
yao ya The Industry.
“Kama
inavyojulikana Aika na Nahreel wana lebo kama walivyo wasanii wengine
ambapo katika lebo hiyo kuna wasanii wachache akiwemo Rosa. Sasa mbali
na kumuweka dada huyo kwenye lebo kumbe Nahreel anatoka naye bila Aika
kujua,” kilisema chanzo.
WAPELEKANA ‘SUPAMAKETI’
Chanzo
kinazidi kutiririka kuwa wawili hao wamezidisha ukaribu na hivi
karibuni wakati Aika akiwa hayupo nyumbani ambapo Rosa huwepo mara kwa
mara kwa ajili ya kurekodi kwa sababu studio na nyumba vipo karibu,
Nahreel alitumia upenyo huo kutoka naye.
“Ilikuwa
ni kawaida yake kumvizia Aika akiwa hayupo, sasa siku hiyo akapata
upenyo na kumuomba Rosa waende naye supamaketi kwa ajili ya manunuzi ya
hapa na pale kisha wapitie kwenye mambo yao, kumbuka wakati huo Aika
hakupewa taarifa yoyote,” kiliendelea kumwaga ubuyu chanzo hicho.
KIMBEMBE CHAANZA
Inadaiwa
walikaa muda mrefu, Aika alifura kwa hasira akiwasubiri kwa hamu maana
alikuwa ameshatonywa kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika uhusiano
huo mchanga.
“Alikuwa
akimsubiri Nahreel arudi aweke wazi amchague yeye ama Rosa lakini
baadhi ya marafiki wa karibu wa Nahreel walikuwa wakimsihi sana
asimfanyie hivyo na asiweke hasira mbele huenda anavyohisi sivyo.”
WAISHI ‘KIBUBUBUBU’
Chanzo
bado kinaendelea kumwaga ubuyu kuwa baada ya Nahreel kurudi, Aika
alishusha mori, alikuwa ameya-elewa maneno aliyo-kuwa akiambiwa na
marafiki wa Nahreel hivyo aliamua kumbadilishia adhabu, kutoka kumuacha
hadi kuishi naye kibubububu.
“Si
Nahreel wala Aika hakuna aliyekuwa akimuongelesha mwenzake ni kama
walikuwa wakiishi kibubububu. Walikaa zaidi ya wiki moja na nusu hakuna
aliyetaka kumuongelesha mwenzake na hata Rosa alikuwa amekalia kuti
kavu,” kilimaliza chanzo hicho.
AIKA HUYU HAPA!
Amani lilimtafuta Aika kujua ukweli ambapo alikiri kuwepo kwa ugomvi huo na kujitetea kuwa walishayamaliza.
“Ujue
mimi na Nahreel tumetoka mbali sana kwa hiyo linapotokea suala la
kukorofishana huwa linatokea kwa muda kisha linaisha, kwa sasa nipo naye
sawa tu jamani,” alisema Aika.
NAHREEL NAYE ANASEMAJE?
Kwa upande wa Nahreel naye alikubali kutokea kwa mvurugano huo na kusema kuwa kamwe hawezi kuja kumuacha mwandani wake huyo.
“Hapa
nilipo nina vidonda vya tumbo hata Aika naye anavyo na hii yote ni
kutokana na kushinda na njaa kipindi cha nyuma tukihangaika pamoja
kutoka. Nampenda na siwezi kumuacha kwa maana migogoro huwa ipo tu,”
alisema Nahreel.
ROSA REE JE?
Rosa
alisema kuwa ni kweli alitoka na Nahreel lakini anamchukulia kama
meneja wake hawezi kujiingiza katika uhusiano wakati anaelewa kuwa
wanaomsimamia ni mabosi zake.
“Vitu kama hivyo huwa vinatokea lakini nashukuru tu vimeisha na maisha yanaendelea.”
AIKA NA NAHREEL NI NANI?
Aika
na Nahreel ni moja ya kapo inayokubalika kwa sasa kwenye Muziki wa
Bongo Fleva. Wawili hao walikutana miaka mitano nchini India ambapo kila
mmoja alikuwa akisomeshwa na wazazi wake. Waliingia katika Kundi la Pah
One lililokuwa likiundwa na wakali kama Ola na Igwe ambapo baadaye
walikuja kutengana na kuamua kutengeneza kundi lao waliloliita Navy
Kenzo.
0 comments:
Post a Comment