Marehemu kwa sasa alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha stefano moshi memorial university college cha mjini moshi, alikuwa anasomea shahada ya sayansi ya habari na mawasiliano mwaka wa pili, aidha alirejea mwanza baada ya kupata likizo kuja kuiangalia familia yake ndipo umauti ukamkuta.
Watuhumiwa sita akiwepo magina selemani ambaye alikuwa na ugomvi na marehemu pamoja na wenzake watano wamekamatwa, wapo katika mahojiano na jeshi la polisi huku uchunguzi kuhusiana na kifo hicho ukiwa bado unaendelea, pindi uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa uchunguzi.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wananchi wa jiji na mkoa wa mwanza, kwamba jeshi la polisi mkoa wa mwanza limesikitishwa na kifo cha askari huyu kwani limempoteza askari kijana ambaye bado jeshi lilikuwa linamtegemea.
Lakini pia anawataka watu wenye tabia za kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga wengine hadi kufikia kupoteza maisha kuwa wanafanya kosa la jinai, na kama watu wanadaiana wafuate taratibu za kisheria zilizowekwa ili kuepusha vifo vinavyoweza kuepukika, hivyo jeshi la polisi linawataka kuacha tabia hiyo mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Imetolewa na:
Dcp: ahmed msangi
Kamanda wapolisi (m) mwanza
0 comments:
Post a Comment