Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Nejembi amewasimisha kazi daktari
mmoja na matabibu wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa tuhuma za
uzembe na ulevi.
Akizungumza
na uongozi wa Mji Mdogo wa Kibaigwa, Ndejembi alisema alikwenda katika
hospitali hiyo ya wilaya usiku akakaribishwa na Televisheni iliyokuwa
inawaka.
“Nilikaa
pale kwa muda wa dakika 45 ndio akatokea mtumishi akasema kuwa alikuwa
katika wodi ya watoto. Lakini unajua tu ipo shida,”alisema.
Alisema kesho yake aliitisha kikao na maazimio yakawa kwamba daktari hayo asimamishwe kazi wakati uchunguzi ukiendelea.
Aliwataja
waliosimamishwa ni daktari wa Meno, Dk Waziri Majuto ambaye
amesimamishwa kwa ulevi na matabibu wawili Daniel Ndahani ambaye
alisimamishwa kwa kukosa weledi wa kazi na Denis Msovero hakuwepo kazini
wakati alipoenda katika hospitali hiyo.
Mwananchi Blog.
0 comments:
Post a Comment