Posted by Williammalecela.com on Friday, August 05, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla leo, - Akagua miradi 6 ya MAJI halmashauri Mbeya - Wakandarasi 5 kati YA 6 wametelekeza miradi YA MAJI
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa siku saba wakandarasi wa
miradi ya MAJI Mkoa wa Mbeya kurudi haraka kukamilisha miradi
waliyoitelekeza kwa kisingizio cha madai ya Fedha Ametoa agizo hilo
leo katka ziara ya kukagua miradi 6 ya MAJI inayolenga kuhudumia Vijiji
17 na kukuta miradi hiyo imetelekezwa na wakandarasi na kufifisha
matumaini ya wananchi kupata huduma ya MAJI Ameagiza wakandarasi
hao kurudi na kuwasilisha certificates za madai yao kwa ajili ya malipo
na ametangaza kuwa wizara ya MAJI kwasasa haiwezi kuleta Fedha mpaka
wapate madai ili waweze kulipa Amesema ameshangaa na amehaidi
kuchukua hatua baada ya kugundua baadhi ya miradi wakandarasi wamelipwa
Fedha Nyingi kuliko kazi zilizofanyika na amesema aina ya wakandarasi
hao wakikaidi kurudi watakamatwa Aidha amewataka wananchi na
viongozi wa maeneo miradi hii inayotekelezwa wasioikee miradi yenye
dosari na ameagiza halmashauri kutokulipa Fedha zote moaka muda wa miezi
sita ya uangalizi wa mradi.
0 comments:
Post a Comment