RAIS wa zamami wa Cuba na Kiongozi mwanamapinduzi, Fidel Castro anasherehekea kutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwake.
Ingawa
Cuba imebadilika sana tangu mdogo wake, Raul Castro achukue madaraka
miaka nane iliyopita, na ushawishi wa Fidel umeshuka, bado anaenziwa
sana na raia wengi wa Cuba. Raul alizaliwa mnamo June 3, 1931 huko huko
Birán nchini Cuba
Hakuna
hafla yoyote rasmi iliyopangiwa kufanywa, lakini Rais wa Venezuela
Nicolas Maduro, taifa mshirika wa karibu wa Cuba, amewasili Havana
kushiriki katika sherehe hizo.
March 21, 2016 rais wa Cuba Raul Castro na rais wa marekani, Barack Obama.
Mtengenezaji sigara maarufu raia wa Cuba ametayarisha msokoto mrefu zaidi wa sigara duniani kwa heshima ya Castro.
Msokoto huo una urefu wa mita 90.
0 comments:
Post a Comment