Dar
es Salaam. Miriam Stephen Mrita (41) amefikishwa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la mauaji ya dada wa bilionea Erasto
Msuya, Aneth Msuya. Wakili
wa Serikali, Diana Lukondo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,
Margareth Bankika kuwa Mei 25, 2016 katika eneo la Kibada, Kigamboni
jijini Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alimuua Aneth.
Baada
ya kusomewa shtaka hilo, Miriam hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu
mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.
Upande
wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na
iliahirishwa hadi Septemba 6. Mshitakiwa alirudishwa rumande kwakuwa
kesi hiyo haina dhamana.
Aneth,
ambaye ni dada wa bilionea Erasto Msuya, aliuawa kwa kuchinjwa na watu
wasiojulikana Mei 25, 2016 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar
es Salaam.
Source:- Mwananchi Blog
0 comments:
Post a Comment