Posted by Williammalecela.com on Friday, August 05, 2016
Msanii wa hip hop Tanzania, Fid Q ambaye atasheherekea siku yake ya kuzaliwa Agosti 13, amesema huenda ataitumia siku hiyo kuachia kazi mpya kwa mashabiki wake.Katika moja ya mahojiano yake Fid Q amesema
kuwa huenda mwaka huu akahadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kuachia
ngoma mbili tofauti na kawaida yake ya kuachia ngoma moja kwa mwaka kwa
kuwa ana mzigo mkubwa wa nyimbo zilizopo kwenye maktaba yake.
“Watu
wangu watarajie kitu cha tofauti na tayari wanaijua tarehe, Agosti 13,
tena stock inavyoonyesha huenda tukafanya double release, lakini tutatoa
tu kwa sababu stock ni nyingi sio kwa sababu ya Presha ya soko, kwa
sababu nimekuwa nikitoa ngoma moja kwa mwaka, nimegundua siku hizi watu
wanaelewa haraka, kwa hiyo ninaweza kuwafanyia mbili kwa mpigo, huwezi
jua”alifunguka Fid.
0 comments:
Post a Comment