Hutakiwi
kushangaa siku ukisikia lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kuwa ipo
juu zaidi ya Mavin Records inayomilikiwa na Don Jazzy, hiyo ni kutokada
na mikakati pamoja na jitihada zinazozidi kuwekwa na uongozi wa lebo
hiyo.
Mpaka sasa lebo ya WCB inawamiliki wasanii wanne
akiwemo Diamond, Harmonize, Raymond na Q Boy Msafi huku kukiwa na
taarifa za chini chini kuwa tayari Rich Mavoko ameshamwaga wino wa kuwa
chini ya lebo hiyo huku bajeti yake ikiwa tayari imeshawekwa pembeni na
tayari amesharekodi wimbo pamoja na video iliyofanyika huko Afrika
Kusini. Lakini pia nje ya kutafuta vipaji kwenye hili analolifanya
Diamond ni biashara kubwa ambayo itafanya akaunti zake za benki kujaa
kila siku.
Hiki ndicho kitaweza kuipaisha lebo ya WCB kuwa kubwa zaidi.
Ukubwa wa jina la Diamond
Hili
halina ubishi kwa sasa Diamond amekuwa ni miongoni mwa wasanii wenye
majina makubwa kwenye tasnia ya muziki kwa Afrika kwa sasa. Hicho ni
kitu ambacho kimemfanya kujitengenezea fan base kubwa kutokana na kazi
zake anazofanya, lakini pia ana uwezo wa kuwatengenezea connection
wasanii wa lebo yake [WCB] kufanya kazi na msanii yeyote wa Afrika
endapo muda utaruhusu kutokana na jina lake huku yeye mwenyewe akizidi
kujitafutia connection za Marekani na Ulaya kama walivyoanza kwa
Harmonize kufanya kazi na Korede Bello kutoka Mavin Records lakini pia
Harmonize aliwahi kusema ana kazi na Kiss Daniel wa Nigeria.
Mashabiki wanaomsupport Diamond
Diamond
ni msanii mwenye washabiki wengi wanaomsupport ambao wapo tayari
kupambana na lolote endapo wataona msanii wao anaandamwa na na maneno
kutoka upande mwingine. Kutokana na hilo uongozi wa WCB unaweza kutumia
pointi hiyo kuifanya lebo yao kuwa juu zaidi kama wanavyofanya sasa kwa
Harmonize na Raymond kutembelea nyota ya Dangote.
Menejimenti ya WCB
Uongozi
wa WCB ukiongozwa na Salaam pamoja na Babu Tale umefanikiwa kufaulu
kwenye suala la mipango na kujiamini kwenye kila wanalolifanya na
hawashindwi kujaribu. Kutokana na uwezo wao walionao wanaweza wakaifanya
lebo ya WCB kufika mbali zaidi lakini itachukua muda mpaka kufika huko.
Source:Bongo5

0 comments:
Post a Comment