Wednesday, August 10, 2016

-Ni malumbano, visasi na kutoshirikiana tangu kuisha uchaguzi 2015
- Awataka wadumishe amani na kutii sheria
- Awahamasisha kujenga sekondari YA mfano ahahidi kuchangia na kushiriki ujenzi
- Rc, ukawa, Ccm wasakata sebene na kuanza maisha YA amani 
- Wananchi WAMPONGEZA na zawadi lukuki
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo ameweka historia katika kata YA Ndanto wilaya YA Rungwe baada ya kumaliza msuguano wa kisiasa uliotokana na uchaguzi Mkuu mwaka jana na kuifanya kata hiyo kuongozwa na Chadema lakini kwa muda mrefu wanachama wenye mlengo tofauti na Diwani wamekuwa na msuguano mkali kiasi cha shughuli za maendeleo kuzorota, Wafuasi wa vyama vya Siasa kulumbana na kufikia kuchomeana ofisi, kungoa bendera na kutoshirikiana ktk mambo YA kijamii
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa amefanya mkutano wa hadhara na kukemea hali hiyo na kuwataka wananchi hao kuacha malumbano na wajikite kwenye maendeleo zaidi na ufundi wa Siasa waweke akiba mpaka mwaka 2020
Amewataka wananchi kumpa ushirikiano Diwani kwakuwa amechaguliwa kisheria na akataka Diwani kuwahudumia wananchi wote bila kuwabagua kwa itikadi zao
Amewataka kuvumiliana, kuheshimiana, kupendana,kushirikiana na serikali itawapa ushirikiano ktk shughuli zote za maendeleo na amewataka kwa kuanzia waanze na ujenzi wa sekondari ya kata na Mkuu wa Mkoa amehaidia kuwaunga Mkono kwa kuwachangia na kushiriki ujenzi jambo lililoibua nderemo na vifijo na kufuatiwa na mziki maarufu disco la nyimbo za Kisafa ambapo Rc, Diwani, Wafuasi wa Ccm , ukawa na wananchi kucheza pamoja kuashiria kumalizika kwa Mgogoro 
Wananchi wengi wamepongeza jitihada za Mkuu wa Mkoa kwani tangu uchaguzi kata hiyo haijawahi kutembelewa na kiongozi

0 comments:

Post a Comment