Monday, August 15, 2016

Afanya ziara za kustukiza kufuatilia maagizo yake YA kuwataka wafanyabiashara kurejea masoko rasmi
 wananchi waeleza urasimu watendaji wa jiji kuwapa vizimba sokoniAtoa siku 7 jiji liwape nafasi kwenye soko la mwanjelwa 
Aongea na madereva wa malori eneo la mafiati atoa wiki 2 wajengewe choo na Maji eneo hilo 
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla Leo amekagua ujenzi wa Barabara za Veta na Block T zinazojengwa bikes kiwango cha lami nakuwataka wakandarasi kujenga kwa kiwango stahiki na hataki kuona Barabara zisizo a viwango mkoani kwake na amehaidi kufuatilia hatua kwa hatua
Aidha amefanya ziara YA kustukiza eneo la Kabwe kufuatilia agizo lake la wafanyabiashara wasio maeneo rasmi wana rejea masoko yaliyo rasmi na kukuta baadhi YA wananchi wanaendelea na biashara kwa kisingizio watu wa jiji wana urasimu wa kuwapa vizimba na Mkuu wa Mkoa amemwagiza mkurugenzi wa jiji ndani YA siku saba awe amewapa vizimba wananchi hao lengo ni kuwaondoa wafanyabiashara hao maeneo hatarishi na kuendeleza kampeni YA usafi
Akiwa eneo la Mafiati ambalo ndilo lin alitumiwa kwa sasa malori YA mizigo amepokea Kero YA kutokuwepo choo ameagiza ndani ya wiki mbili ujenzi wa choo ukamilike eneo hilo
Amewataka wananchi kushirikiana na serikali kuhakikisha jiji litakuwa katika hali ya usafi . " Ndugu zangu nataka mnielewe nataka kila mmoja wetu aelewe nia Nzuri niliyonayo nataka jiji safi , kila Mwananchi afanye biashara eneo zuri lenye uhakika na biashara na kama kuna urasimu wa kupewa vizimba niambieni Nipo kwa ajili yenu."
Akiwa eneo la tukio maafisa wa jiji walikuwa wakihaha kuwaandikisha wananchi ili kuwapa vizimba sokoni

0 comments:

Post a Comment